29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Azam FC yazitaka pointi tatu kwa Namungo

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

KOCHA Msaidizi wa Azam FC Vivier Bahati, amesema watahakikisha wanaondoka na alama tatu katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo utakaopigwa kesho kwenye Uwanja Azam Complex, Dar es Salaam.

Azam inashuka dimbani ikiwa imetoka katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids ambao wametoka suluhu, huku ikiwa haina matokeo mazuri ya Ligi Kuu.

Kocha Mkuu wa Azam FC, Gerge Lwandamina.

Azam haijapata ushindi katika michezo yake miliwi ya Ligi Kuu iliyoanzia ugenini, ikitoka sare ya 1-1 na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, kisha kufungwa 2-1 na Polisi Tanzania kwenye dimba la Ushirika mjini Moshi.

Akizungumzia mchezo huo leo Oktoba 18, Bahati amesema kikosi kipo vizuri kwa mapambano kwani matokeo waliyopata katika mechi mbili zilizopita si mazuri kwa timu kama Azam.

“Tumetoka mechi ya Kimataifa, tunarudi katika ligi, tumepata siku mbili za maandalizi, tunahitaji pointi tatu za kesho ili kutupa njia. Kazi kubwa tulifanya katika mazoezi ni eneo la ushambuliaji kwa sababu nafasi tunapata lakini wachezaji wanashindwa kutumia,” amesema Bahati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles