30 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

“Uzeni hata nyumba zenu, ninachotaka wakulima wa tumbaku walipwe”- Bashe

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe amegeuka mbogo kwa kuzigomea kampuni tano za wazawa zinazonunua tumbaku kutoondoka ofsini kwake hadi wasaini kwa maandishi ni lini watamalizia deni la wakulima wa zao hilo la zaidi ya Sh bilioni 4.

Pia amesema Serikali haitayaruhusu makampuni hayo kuendelea kununua tumbaku kwa wakulima msimu ujao iwapo haitawalipa deni hilo.

Akizungumza leo Februari 11,2022, jijini Dodoma katika kikao chake na kampuni hizo, Waziri Bashe amesema haiwezekani mkulima akae shambani zaidi ya miezi 10 halafu aje adhulumiwe fedha zak,e hivyo amezitaka kampuni hizo kuhakikisha zinalipa madeni ya wakulima hao kwa kuweka makubalino kwa maandishi.

Amesema wamiliki wa kampuni hizo ikiwezekana wauze nyumba zao ili waweze kulipa madeni hayo.

Tumbaku

Bashe amesema Serikali imefanya juhudi kuhakikisha inayasaidia kampuni hizo lakini anashangaa ni kwanini zimeshindwa kumalizia deni hilo.

“Hapa haondoki mtu mpaka nijue hela ya mkulima inapatikanaje, sitaki stori nataka Commitment inayomaanisha, ikiwezekana kauze nyumba yako nataka hela ya wakulima, hapa huondoki mtu bila kuacha alama ya maandishi na kila mmoja asaini hiyo hela inalipwa lini,”amesema Waziri Bashe.

Waziri Bashe amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa kampuni hizo lengo likiwa ni kumsaidia mkulima aweze kujikwamua kiuchumi.

Pia amesema serikali haitaruhusu kampuni hizo kuendelea kununua tumbaku kwa wakulimu msimu ujao iwapo haitawalipa wakulima deni hilo.

“Hatuwezi kuondoa umaskini bila ya kuwasaidia Watanzania. Hatutamruhusu mtu kuingia kwenye masoko kama hujamaliza deni,”amesema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Bodi ya Tumbaku, Stanley Mnovya amesema kati ya kampuni nane zilizopitishwa na serikali kwa ajili ya kununua tumbaku kwa wakulima ni tatu tu zilizokamilisha malipo yawakulima.

Amesema wameweza kulipa zaidi ya Sh bilioni 28 ambapo kampuni tano bado zinadaiwa Sh bilioni 4.8,  hivyo amewataka kuweka makubaliano ni lini watamaliza deni hilo.  

Naye, Mkurugenzi wa kampuni ya  Jespan Co. Ltd, George Geremiah amewaomba radhi wakulima wa zao hilo huku akiahidi watamaliza deni hilo katika muda ambao watakuwa wamepanga.

“Tunaomba radhi tunaomba wakulima waendelee kutusamehe,”amesema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kampuni ya Pach-Tech, Charles Muhikwa amesema amesikia maelekezo ya Waziri na kampuni yake ipo tayari kulipa deni hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles