23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

UVUVI HARAMU WAKWAMISHA SOKO LA KIMATAIFA

Na FERDNANDA MBAMILA–DAR ES SALAAM


Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, imekuwa ikipiga  vita suala la uvuvi haramu.

Wavuvi hufanya shughuli hizo kwa kutumia tindikali na baruti kuvulia samaki kutokana na hali ngumu ya maisha kuwakumba  na inawawia vigumu sana  kupata vifaa vya kisasa.

Hatimaye wavuvi hao kutumia zana haribifu za kuvulia na kusababisha  uharibifu wa samaki na mazingira kwa ujumla.

Pia nyenzo na vitendea kazi vya kuvulia samaki  vinavyotumika hadi leo ni vya teknolojia  ya muda mrefu ambavyo havina ubora na uwezo wa kuvuna samaki wengi. Hali hiyo huchochea kukosa ajira  kwa vijana na hivyo  kukosekana kwa bidhaa ya samaki katika nchi mbalimbali wakati rasilimali zipo nchini.  Kwa upande mwingine,  Serikali wangezingatia upatikanaji  kwanza  wa vifaa vya kisasa vya kuvulia samaki kwa wavuvi.

Vilevile Wizara ina wajibu wa kujua matatizo na maendeleo  ya wavuvi  kwa kuwa na utaratibu mzuri wa kuwatembelea na kujua  hali yao popote pale ili kuwaweka katika mazingira  bora  na yakiteknolojia ya utumiaji wa vifaa vya kuvulia vya kisasa kulingana na masoko ya kimataifa katika uuzwaji wa samaki.

Ingawa  kwa asilimia chache sana  samaki huuzwa  nje ya nchi na ipo nyuma katika uzalishaji wa bidhaa ya samaki kwa wingi.

Hivyo, taifa kushindwa kufikia malengo stahiki  ya mpango  mkakati wa maendeleo ya  nchi ya viwanda.

Hali hiyo vilevile inawakumba wavuvi wa Soko la Kimataifa la Feri kutokuwa  na vifaa vya kisasa  kwa ajili uvuvi wa samaki na hivyo kusababisha kutumia mbinu mbadala  na haribifu ambayo inawawezesha kupata samaki kwa urahisi zaidi.

Inasikitisha kuona kuwa kwa asilimia kubwa sana ya wavuvi hapa nchini hutumia baruti kuvulia samaki.

Wavuvi  hao wa  Soko Kuu la Kimataifa la Feri wameiomba Serikali kuwapatia mikopo ya fedha ili waweze kununua vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuvulia samaki, jambo ambalo linaweza kuwasaidia kuendesha shughuli zao kwa urahisi na salama zaidi.

Naye  Naibu katibu wa Soko hilo, Abeid  Bura, anasema kuwa endapo Serikali watalitilia mkazo suala hili linaweza kuwasaidia baadhi yao kuondokana na uvuvi haramu na kuingia kwenye uvuvi wa kisasa ambao utawasaidia kuongeza uzalishaji wa mazao ya samaki na kukuza kipato.

“Changamoto kubwa tuliyonayo ni pamoja na ukosefu wa vitendea kazi vya kisasa kwa ajili ya kuendesha shughuli zetu, jambo ambalo limesababisha baadhi yetu kutumia uvuvi haramu kwa ajili ya kupata samaki,” anasema Bura.

Anasema  vyombo vinavyotumika sasa hivi kuvulia samaki ni vile vya kizamani ambavyo vinasababisha  wavuvi kutumia  njia rahisi ikiwamo ya uvuvi haramu ili kukidhi  mahitaji  yao.

Anasema kutokana na hali hiyo, wameiomba  Serikali  kuwapatia mikopo  ambayo itawasaidia kununua vifaa vya kisasa  kama vile nyavu na boti za kisasa  za kuvulia samaki.

Anasema kutokana na hali hiyo, mikopo hiyo itawasaidia kupata vifaa bora ambavyo vitaweza kuongeza uzalishaji wa samaki na kuisadia Serikali kupata mapato.

Pia itaisaidia Serikali kujulikana katika soko la kimataifa kutokana na uboreshwaji wa mazingira mazuri kwa wavuvi na  vifaa vya kisasa.

Hii itakuwa chachu  kwa wateja wa mataifa mbalimbali kutokana na kuuziwa bidhaa bora na salama kutoka Tanzania isiyovuliwa kwa kemikali na madawa mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles