DIAMOND: 20 PERCENT AKIHITAJI KUSAIDIWA NITAMSAIDIA

0
906

Na GLORY MLAY


MSANII wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, amesema ana uwezo wa kumsaidia msanii 20 Percent ili arudi tena kimuziki na kuwa tishio kama mwaka 2011, lakini hadi atake kusaidiwa.

Diamond alisema wapo wasanii wanaohitaji msaada katika kazi zao na wanaonyesha utayari wa kusaidiwa, lakini wapo pia wanaohitaji msaada lakini hawaonyeshi utayari wa kusaidiwa.

“Kuna wasanii wanakufuata, anakwambia nimeshindwa hapa, nimekwama nisaidie unamsaidia lakini wapo wanaohitaji msaada lakini hawaonyeshi kusaidiwa kama 20 Percent, siwezi kumfuata na kumwambia nataka nimsaidie kimuziki lakini kama anataka kusaidiwa, nitamsaidia akionyesha kutaka kusaidiwa,” alisema.

Diamond aliongeza kwamba yupo tayari kumsaidia msanii yeyote aliyekwama kwenye kazi zake na anayeonyesha nia ya kutaka msaada.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here