23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

TANESCO YAPONGEZWA KWA KAZI NZURI, LINDI TATIZO HALIPO

Na Mwandishi Wetu


MAMBO mengi makubwa yalifanywa wakati wa ziara ya Rais Dk. John Magufuli mkoani Mtwara, lakini hayakupewa uzito unaostahili ikiwemo uzinduzi ya miradi ya Shirika la Umeme (Tanesco) ambayo inawahakikishia upatikanaji umeme wa uhakika wakazi  wa Lindi.

Rais Dk. Magufuli alizindua Kituo cha kupoza umeme cha Tanesco kilichoko mjini Mtwara, ambacho kimejengwa na wataalamu wa Tanesco kwa gharama ya Sh bilioni 16, mradi ambao utahusisha ujenzi wa njia ya umeme ya kilovoti 132, kutoka Mtwara hadi Lindi, hivyo kumaliza tatizo la kukatika katika kwa umeme katika Mji wa Lindi.

Rais Magufuli alimpongeza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, menejimenti na wafanyakazi wa Tanesco kwa kazi nzuri wanayofanya iliyowezesha usambazaji wa umeme nchini kuongezeka hadi kufikia asilimia 46 nchi nzima.

Alisema matokeo hayo ni mazuri kwa muda mfupi uliotumika na kuona kuwa kama wakijibidisha wanaweza kufika mbali. Kwa msingi  huo  alitoa maagizo kwa Tanesco kuwakatia umeme wote wenye madeni bila kujali kama ni taasisi ya umma ama binafsi na kunyambua neno la kata katika muundo wake wa ka==tan, kata na  hivyo kuwavutia watu wengi.

Alisema Serikali na idara zake zote zinazo  bajeti ya umeme na hivyo haoni sababu ya wahusika kutotia maanani kulipa ankara za Tanesco, wakati umeme wanatumia na kusababisha matatizo ya utekelezaji miradi yake.

Alilaani tabia iliyojengeka nchini ya kubadili mafungu ya pesa  za umma na kutumia pesa kinyume na taratibu zilizopangwa na kufanya miradi mingi isifanikiwe vilivyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles