23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Utata waghubika maofisa wa CAG

assadNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

UTATA umejitokeza kuhusu hatima ya maofisa wa Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambao wanatuhumiwa kuhongwa na wakurugenzi.

Pamoja na hali hiyo, maofisa hao wanadaiwa kuhongwa na baadhi ya wakurugenzi wa halmashauri nchini.

Taarifa ambazo MTANZANIA inazo zinaeleza kwamba wafanyakazi hao walikabidhiwa barua ya kusimamishwa kazi Februari 18  mwaka huu.

Hiyo ilikuwa  siku moja baada ya waziri George Simbachawene kuelezea kuwasimamisha kazi wakurugenzi wanne na kuzitaka mamlaka nyingine kuchukua hatua stahiki kwa wafanyakazi wao.

“Nimeona taarifa katika gazeti lenu kuwa bado tunaendelea na kazi… nikuambie wazi kama ulivyoelezwa ofisini kwetu mimi nimepumzishwa kupisha uchunguzi na nimepewa barua Februari 18.

“Sasa sijui hao wanaoendelea na kazi kwa mujibu wa CAG ni kina nani,” alihoji mmoja wa waliosimamishwa

Barua ya kuwasimamisha kazi wafanyakazi wa ofisi ya CAG walitajwa katika taarifa ya Waziri George Simbachawene, iliyoripotiwa Februari 11  mwaka huu, ikiwa ni siku sita kabla ya taarifa hizo kutolewa hadharani.

Hata hivyo, mmoja wa wakaguzi waliotajwa kuhusika na kadhia hiyo, Stephen Owawa, alisema ameshangazwa na taarifa  hiyo wakati hajawahi kufanya kazi mkoani Kagera na hakuwahi kufanya ukaguzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi.

Owawa ambaye aliacha kazi katika ofisi ya CAG Agosti 24 mwaka jana baada ya kupitishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema)  kuwania ubunge katika jimbo la Rorya, alisema ni wakati muafaka kwa mawaziri kupata taarifa sahihi kabla ya kuzitoa hadharani.

“Mimi niliomba likizo kuanzia Juni mwaka jana baada ya kupitishwa na chama changu kuwania ubunge Rorya  na niliacha kazi Agosti 24  mwaka jana.

“Nimesikia taarifa ya waziri inasema tuhuma hizo ni za Septemba, ina maana hawajui kama wakati huo sikuwa kazini bali nilikuwa katika kampeni?” alisema Owawa.

Alisema  kwa ukaguzi wa mwaka 2014/2015 ripoti yake inatakiwa itoke Machi mwaka huu na kwamba katika kipindi chote cha utumishi wake hakuwahi kukagua hesabu za Wilaya ya  Misenyi.

Februari 22  mwaka huu, CAG Profesa Assad,  aliimbia MTANZANIA kwamba hadi    sasa bado hajawachukulia hatua zozote watumishi hao kwa kuwa hajapata barua kutoka kwa mamlaka husika.

Alisema  akiipata atafanya   kama ilivyoshauriwa na Waziri Simbachawane.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles