30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Uchaguzi wa Meya Dar kesho

simbaaKOKU DAVID NA FLORIAN MASINDE, DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene, amesema  uchaguzi wa Meya wa   Dar es Salaam unatarajiwa kufanyika kesho.

Akizungumza   na MTANZANIA jana, alisema  ofisi yake imemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam  kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika Februari 29  mwaka huu na kuusimamia kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa jiji.

Simbachawene alikuwa akitoa ufafanuzi kuhusu mipaka ya utendaji kazi wa mameya na wakuu wa wilaya ambako hivi karibuni  ulitokea mgogoro kati ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda na Meya wa Manispaa hiyo, Boniface Jacob.

Waziri  alimtaka mkuu huyo wa wilaya kuacha kuingilia majukumu ya Baraza la Madiwani.

Simbachawene alisema   Mkuu wa Wilaya ndiye msimamizi mkuu wa shughuli zote za Serikali ikiwa ni pamoja na zile za maendeleo katika wilaya husika.

Alisema pamoja na hayo ndiye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama kwa mujibu wa sheria na anaweza kuingilia uamuzi wa vikao vya madiwani iwapo hautakuwa sawa kwa ajili ya maendeleo.

“Meya yeye ni mwenyekiti wa baraza la madiwani, mchochezi wa mikutano ikiwa ni pamoja na usimamizi mkuu wa vikao vya kamati za fedha za wilaya.Alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles