26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Usiku wa Ulaya kuendelea leo

Diego SimeoneMADRID, HISPANIA

USIKU wa Ulaya unatarajia kuendelea leo katika viwanja viwili, cha Vicente Calderon, Atletico Madrid watawakaribisha Barcelona, huku Benfica wakiwa kwenye uwanja wao wa Estadio da Luz na kuwakaribisha Bayern Munich.

Mchezo wa awali ambao ulipigwa Nou Camp, Atletico walipokea kichapo cha mabao 2-1, hivyo leo hii wana kazi ngumu ya kuweza kutamba katika mchezo huo.

Barcelona watahakikisha wanashinda mchezo huo kwa kutoa sare ya aina yoyote ili kuweza kusonga hatua ya nusu fainali, wakati huo Atletico ikihitaji ushindi wa zaidi ya bao moja.

Kwa ubora walionao Barcelona bado wana nafasi kubwa ya kushinda kwa kuwa wanautolea macho mchezo huo kwa ajili ya kutetea ubingwa huku wakiwa na uhakika wa kutetea na Ligi Kuu.

Kocha wa Barcelona, Luis Enrique, amedai kwamba macho yao wanayaelekeza katika mchezo wa leo hivyo lazima waibuke na ushindi dhidi ya kukosi cha Diego Simeone.

Wakati huo mchezo mwingine ni kati ya Benfica ambao watajaribu kuutumia uwanja wao wa nyumbani.

Katika mchezo wa awali, Bayern ilifanikiwa kushinda bao 1-0 katika dakika ya pili ya mchezo huo ambapo lilidumu hadi dakika 90 zinamalizika.

Mchezo huo ulionekana kuwa mgumu wa Bayern japokuwa walikuwa nyumbani, hivyo tunatarajia kuona ugumu zaidi huku Benfica wakiwa nyumbani leo hii.

Hata hivyo, kocha wa Bayern, Pep Guardiola, amedai kwamba atahakikisha anaingia hatua ya nusu fainali ili kujihakikishia anatwaa ubingwa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles