Rais huyo aliondolewa madarakani Alhamisi iliyopita baada ya mahakama moja ya Jos kuamua kuwa kiongozi huyo alishindwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2014.
Mahakama ilisema kuwa Chris Giwa ndiye anayefaa kuwa Rais wa Shirikisho la Soka Nigeria (NFF) na si Pinnick.
Fifa imeionya vikali Nigeria na kuiambia kwamba ipo katika hatari ya kufungiwa endapo itatekeleza uamuzi wa mahakama.
Katika taarifa iliyotumwa kwa Serikali ya Nigeria, mwanzoni mwa wiki hii, Kaimu Katibu wa Fifa, Markus Kattner, anasema uamuzi huo wa mahakama unatafsiriwa kama kuingilia kati katika masuala ya soka.
”Bila shaka uamuzi wa mahakama hiyo ya Jos unatafsiriwa kuwa ni kuingilia uendeshaji wa shirikisho na bila shaka inakiuka kanuni za Fifa ambazo haziruhusu masuala ya soka kuamuliwa mahakamani,” alisema Kattner.
Inadaiwa kwamba sio mara ya kwanza kwa Chris Giwa kwenda mahakamani kutafuta suluhu ya mgogoro wa usimamizi wa shirikisho la soka la Nigeria.
Mwaka uliopita pia alikwenda katika mahakama ya michezo ambapo alishindwa katika uamuzi uliotolewa.
Tofauti hizo zinaiweka Nigeria ‘Super Eagles’ katika hatari kubwa ya kupigwa marufuku katika mashindano hayo yatakayofanyika huko Rio de Jenairo na vile vile kuharibu maandalizi yao ya kuelekea Kombe la Dunia 2018.