23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Toyin: Nisipoolewa na Mzungu basi

Toyin-AimakhuLAGOS, NIGERIA

NYOTA wa filamu nchini Nigeria, Toyin Aimakhu, ameweka wazi kwamba asipoolewa na Mzungu basi ataishi bila kuolewa.

Mrembo huyo amedai kwamba ndoto zake katika maisha ni kuja kuolewa na Mzungu na sio mwanaume kutoka Afrika.

“Kila mtu ana ndoto zake, katika maisha yangu nimepanga kuolewa na Mzungu na kama ikishindikana sitaolewa.

“Najua wanaume ni wengi lakini sina mpango wa mwanaume wa Kiafrika.

“Niliwahi kuolewa sikukaa sana katika ndoa yangu kwa kuwa mwanaume huyo alikuwa anapenda sana wanawake nikaondoka ndio maana sioni sababu ya kuolewa na mtu wa Afrika,” alisema kupitia akaunti yake ya Instagram.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles