28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Ciara apata kigugumizi kutaja jina la Future

Ciara,,NEW YORK, MAREKANI

MKALI wa muziki nchini Marekani, Ciara Harris, juzi alijikuta akiwa na kigugumizi wakati wa utoaji tuzo za Billboard.

Ciara alipata nafasi ya kuwataja wasanii wa hip hop wanaowania tuzo hizo huku likiwemo jina la mpenzi wake wa zamani Future.

Ciara alipata nafasi hiyo akiwa na mkali wa hip hop, Ludacris, lakini watu walimshangaa kwa kuhangaika kulitaja jina la Future baada ya kukamilisha kuyataja majina mengine ya Drake na Fetty Wap, huku jina la tatu likiwa la Future.

Ciara na Future walifanikiwa kupata mtoto mmoja baada ya kuvishana pete Oktoba 2013, lakini uhusiano huo ulivunjika Agosti 2014.

Kwa sasa, Ciara yupo na mchumba mpya ambaye ni mwanamichezo anayejulikana kwa jina la Russell Wilson ambao uhusiano wao ulianza Julai 2015.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles