28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Mashabiki Moro, Dar waanza kubeti shoo ya madansa

Ngedere, Chini ni Mc CoolNA BEATRICE KAIZA

WAKATI wanenguaji wa zamani katika miaka ya 80 wa Mkoa wa Morogoro na wa Dar es Salaam wakiwa katika mazoezi makali ya kujiweka sawa kimwili, mashabiki na wadau wa wanenguaji hao wameanza ‘kubeti’ washiriki wa mkoa utakaoshinda.

Mashabiki hao walionekana kukamiana huku wa Morogoro wakiwalazimisha wa Dar es Salaam waweke fedha zitakazonyakuliwa kwa mashabiki wa mkoa utakaoshinda.

Onyesho hilo maalumu la ujirani mwema linatarajiwa kufanyika Aprili 24, katika Ukumbi wa Samaki Samaki Kihonda Morogoro.

Mchanganyiko wa wanenguaji hao utawakilishwa na kiongozi wa wanenguaji Mkoa wa Morogoro, Maneno Ngedere na washiriki wenzake Bob Tiger, Zumba Cool, Loger Loger na wengine huku Mkoa wa Dar es Salaam ukiongozwa na mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Mipango wa Chama cha Wacheza dansi nchini (TDA), Salum Makuka ‘Sammy Cool’.

Wanenguaji wengine kutoka Dar es Salaam ni Mc Cool, Ommy Sidney, Bosco Cool Jay, prodyuza Baucha, Kelly John, Athuman Diga Diga, Bob Richie, Small Jobiso, Mzee Bachu, Super Convoy, Hamad Sweet Kajela na wengine wengi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles