28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Ushuzi wasimamisha Bunge Kenya

NAIROBI, KENYA 

MJADALA  mkali juu ya hali ya masoko ulikatizwa ghafla kwa harufu kali ya ushuzi.

Kadhia hiyo haikutokea sokoni ama mtaani, bali ni kwenye ukumbi wa Bunge la Kaunti ya Homa Bay, Magharibi kwa Kenya.

“Mheshimiwa Spika, mmoja wetu hapa amechafua hali ya hewa,” alisema Julius Gaya kwenye kikao cha Bunge.

Lakini mjumbe aliyerushiwa lawama za kujamba alikanusha vikali akisema: “Sio mimi. Siwezi fanya kitendo kama hicho mbele ya wenzangu.”

Katika jitihada za kupambana na harufu hiyo, Spika Edwin Kakach akaamuru wajumbe wote watoke nje kwa muda.

Ripoti pia zinaeleza kuwa aliagiza marashi ili kuleta harufu nzuri. “Lete (marashi) ya aina yeyote utakayoyakuta ofisini kwangu.

hatuwezi kuendelea kukaa kwenye mazingira ya kunuka.”

Hata hivyo inadaiwa harufu hiyo ilikatika kabla ya marashi hayo kupatikana hali iliyoruhusu kikao kuendelea.

Inaripotiwa kuwa tukio hilo la kipekee lilitokea Jumatano wiki hii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles