MKALI wa RnB nchini Marekani, Usher Raymond, amefanikiwa kufunga ndoa na mpenzi wake, Grace Miguel.
Grace ni Meneja wa msanii huyo, ambapo walianza uhusiano wa kimapenzi tangu mwaka 2009 baada ya msanii huyu kubwagana na mpenzi wake, Tameka Foster, mwaka huo.
Tameka alifanikiwa kupata watoto wawili wa kiume na msanii huyo ambao wanajulikana kwa majina ya Usher V na Naviyd Ely.
“Alikuwa meneja wangu kwa kipindi kirefu, lakini kwa sasa naweza kusema kuwa ni mke wangu, alinisaidia sana katika kazi zangu za muziki, kuna wakati nilikuwa na hali ngumu katika muziki ila aliniokoa kwa kiasi kikubwa na nikaona niwe naye katika maisha yangu,” alisema Usher.