24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

URAIS UFARANSA NI MACRON, LE PEN

PARIS, UFARANSA


MGOMBEA wa siasa za mrengo wa kati, Emmanuel Macron na mgombea wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, Marine Le Pen, watachuana katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa.

Kwa mujibu wa matokeo ya kura, Macron amepata asilimia 23.9 ya kura na Le Pen alipata asilimia 21.4. 

Kura za maoni zilizochapishwa juzi zinaonyesha Macron atamshinda Le Pen kwa urahisi katika duru ya pili.

Akihutubia baada ya ushindi wake hapo juzi, Macron alisema tangu kuundwa kwa jumuiya yake ya kisiasa mwaka mmoja uliopita, siasa za Ufaransa zimebadilika. 

Alisema anataka kuwa rais wa wote, ambaye atawezesha watu wanaotaka kuwa wabunifu na wenye ari ya kutenda kazi ili kuyafikia malengo yao kwa urahisi na haraka zaidi. 

Marine Le Pen kwa upande wake, aliwataka Wafaransa waitumie fursa ya kihistoria iliyopo kumwingiza madarakani.

Le Pen alisema wakati umefika wa kuwakomboa Wafaransa kuondokana na kiburi cha tabaka la watawala.

Mgombea wa Chama cha Kisoshalisti, Benoit Hamon, Waziri Mkuu wa Ufaransa, Bernard Cazeneuve na mgombea urais wa chama cha kihafidhina, Francois Fillon walioshindwa kuingia duru ya pili, wametoa wito kwa wapigakura kumuunga mkono Macron katika uchaguzi wa duru ya pili.

Ufaransa inakabiliwa na mvutano kati ya pande mbili baina ya Macron anayetetea sera ya Umoja wa Ulaya (EU) na Marine Le Pen anayepinga EU na sera za uhamiaji.

Le Pen aliahidi kufanyika kura ya maoni juu ya Ufaransa kuendelea kuwamo au kujiondoa EU, akiiga hatua zilizoshuhudia Uingereza ikiondoka katika umoja huo. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles