29.9 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

UPELELEZI KESI YA AKINA MASAMAKI FEBRUARI

Na KULWA MZEE-DAR ES SALAAM


Tiagi MasamakiTAARIFA ya upelelezi katika kesi ya kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 12.7 inayomkabili Tiagi Masamaki na wenzake inatarajiwa kutolewa Februari mwaka huu.

Hayo yalidaiwa jana na Wakili wa Serikali, Vitalis Peter, wakati kesi hiyo ilipokuwa ikitajwa na kwamba upelelezi haujakamilika, hivyo aliomba apewa muda wa kueleza hatua ya upelelezi ilipofikia wiki ijayo.

Akiwasilisha ombi hilo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, Wakili Peter alidai maelekezo aliyonayo ni kwamba watakuja kutoa hatua ya upelelezi ilipofikia wiki ijayo.

Wakili huyo aliomba kesi hiyo iahirishwe hadi wiki ijayo. Hakimu alikubaliana na ombi hilo, hivyo aliahirisha kesi hadi Februari 3, mwaka huu na dhamana za washitakiwa zinaendelea.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 12.7 ni Mkuu wa Kituo cha Huduma kwa Wateja TRA, Habibu Mponezya na Meneja Udhibiti wa Forodha na Ufuatiliaji, Burton Mponezya, Haroun Mpande wa Kitengo cha Mawasiliano  ya Kompyuta (ICT TRA) na Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara TRA, Hamis Omary.

Wengine ni wafanyakazi wa Bandari Kavu (ICD) ya Azam ambao ni Msimamizi Mkuu wa Kitengo cha Ushuru wa Forodha, Eliachi Mrema, Meneja wa Operesheni za Usalama na Ulinzi, Raymond Louis na Meneja, Ashraf Khan.

Masamaki na wenzake walipandishwa kizimbani Desemba 4, mwaka juzi, wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, kwa kula njama ya kudanganya na kuisababishia Serikali hasara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles