32.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

UNDP, Tony Elumelu kusaidia wajasiriamali 100,000 Afrika

Niamey, Niger

MRADI wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP), umeungana na Taasisi ya Tony Elumelu (TEF), kwa ajili ya kutoa mafunzo, muongozo na fedha kwa wajasiriamali wadogo 100, 000 kutoka barani Afrika ili kuendana na Mpango wa Maendeleo Endelevu (SDGs) na ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika.

TEF na UNDP zimeungana kupitia Programu ya Wajasiriamali Wadogo ya Sahel, ambayo imekusudia kuhimiza sapoti ya biashara,  lengo likiwa ni kuendeleza mamilioni ya nafasi mpya za kazi na angalau kutoa Dola za Marekani bilioni 10 katika pato la Afrika.

Hayo yamesemwa leo na Julai 9, na Muasisi wa TEF, Tony Elumelu katika Mkutano wa 12 wa Baraza la Umoja wa Afrika, ambao pia uliudhuriwa na Mkurugenzi wa UNDP Afrika, Ahunna Eziakonwa na baada ya Marais wa Afrika kukutana na  kutia saini mkataba wa kuzindua biashara huru barani Afrika Rais wa Niger alishiriki kuzindua program hiyo ya Sahel.

Elumelu amesema ushirika huo utalenga kuinua vijana wadogo wa Afrika ambao wanatokea katika jamii za hali ya chini, kwa kuanza na program ya Sahel itatoa nafasi kwa bara la Afrika ambalo linatajwa kuwa na watu na idadi ndogo ya watu ikikadiriwa kuwa  vijana chini ya miaka 25  milioni 194 ambayo ni sawa na asilimia 64.5% ya watu wote.

“Programu hii imeshawanufaisha wajasiriamali wadogo 7,520 katika miaka mitano tangu kuanzishwa kwake katika nchi 54 za Afrika, mbali na hiyo pia inalenga kuwakutanisha vijana hao ili wabadilishane uzoefu wa biashara lengo likiwa ni kutengeneza ajira mpya na kwa ukuaji wa uchumi jamii wananazotoka na nchi kwa ujumla,“ amesema Elumelu.

Naye Mkurugenzi wa UNDP Afrika, Ahunna amesema wanaiangalia program ya Sahel kama uwanja wa fursa na kuwekeza kwa vijana wadogo ni kuimarisha bara la Afrika.

“Vijana wanatakiwa kuwa kama moyo au kiini cha ajenda yoyote ya maendeleo, tunahitaji kuwekeza katika akili, nguvu, ubunifu na vipaji ili kutengeneza fursa za wao kufikia ndoto zao nah ii nidyo sababu UNDP kuingia katika program ya Sahel ili kuwekeza katika maendeleo endelevu, nitoe wito kwa sekta binafsi pia kuungana na TEF kuawsapoti wajasiriamali wadogo,” amesema Ahunna.

 Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa TEF, Ifeyinwa Ugochukwu amesema : “Ushirika wetu na UNDP utasaidia mafanikio ya wajasiriamali wengi na huu ni ushuhuda kuwa taasis yetu imefanya mambo mengi, Afrika inahitaji washirika sio tu wanaoamini katika sekta binafsi ila kuja na ahadi kama hizi, UNDP imethibitisha kuwa washirika wetu wa kweli tutafanya nao kazi kuhakikisha tunaondoa umaskini Afrika.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles