24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, March 29, 2023

Contact us: [email protected]

Mobetto haumizwi na mitandao ya kijamii

Na Brighiter Masaki

MSANII wa Bongo Fleva, Hamisa Mobetto, ameweka wazi kuwa, hana muda wa kufuatilia kinacho andikwa kwenye mitandao ya kijamii juu yake.

Msanii huyo amedai, mitandao ya kijamii imekuwa ikiandika habari nyingi ambazo hazina maana na zingine zinaweza kukupotezea muda wako kuzifuatilia.

“Husipokuwa makini na mitandao ya kijamii utaumia, watu wanapenda kuandika habari ambazo hazina ukweli lakini zinapendwa kufuatiliwa na wengi.

“Kwa sasa sina muda huo wa kuangalia watu wanasemaje juu yangu kwenye mitandao ya kijamii, nitapoteza muda bure wakati nina mambo mengi ya kufanya katika maisha yangu, naacha watu waendelee kupoteza muda wao,” alisema mrembo huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,259FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles