25 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

UFINYU WA BAJETI KIKWAZO UZAZI WA MPANGO

Na ANDREW MSECHU-DAR ES SALAAM


KUTOTEKELEZWA kwa bajeti kumetajwa kuwa suala linalochangia kuzorotesha juhudi za kusimamia uhamasishaji wa uzazi wa mpango, kutokana na Serikali kutoa kiasi kidogo  cha fedha tofauti na matarajio na mahitaji ya huduma hizo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mtaalamu wa Utetezi wa Mama na Mtoto wa kituo cha Mawasiliano Chuo Kikuu cha John Hopkins, James Mlali, alisema kwa sasa bajeti ya nchi bado haijafikia kiwango cha kukidhi mahitaji ya kutoa huduma hizo.

“Tunaona mwaka wa fedha uliopita, yaani 2017/18, Serikali ilipanga kutoa Sh bilioni 14 lakini haikuweza kutoa hata nusu yake, ilitoa Sh bilioni mbili pekee kwa hiyo utekelezaji wa mipango uliathiriwa,” alisema.

Alisema athari hizo zimeendelea kuwapo kila mwaka na hata wakati mwingine Serikali inapotoa kiasi hicho kidogo cha fedha   hutolewa mwisho wa mwaka wakati mipango ilitakiwa kuendelea kwa mwaka mzima.

Mlali   alikuwa akizungumza kuelekea maadhimishio ya kimataifa ya Siku ya Uzazi wa Mpango Duniani inayoadhimishwa Septemba 26 kila mwaka.

Alisema suala la uzazi wa mpango lina mchango kwa maendeleo ya nchi na kwa sasa inaweza kuchangia katika kufikia Tanzania ya viwanda kwa kuwezesha ushiriki mkubwa wa wanawake katika kuchangia ujenzi wa uchumi.

Alisema kwa sasa kuna maeneo ambayo hayana vituo vya kutoa huduma za uzazi wa mpango na vingine vyenye huduma hizo zinatoa huduma kwa wachache kwa hiyo kutofikia wananchi wengi.

Mlali alisema kwa sasa ni wazi kwamba huduma za uzazi wa mpango kwa njia za asili ambazo zimekuwa zikitumika tangu enzi ufanisi wake umekua hafifu kutokana na sababu kadhaa.

Alisema  njia za kisasa zimekuwa na ufanisi kutokana na matokeo ambayo uyamethibitishwa kwa utaalamu.

Alisema njia za kisasa zina ufanisi zaidi kwa wanaotaka kupanga uzazi kwa watu wanaopanga familia kwa kuwa na idadi ya watoto wanaowahitaji ili wajikite katika shughuli za uzalishaji mali kwa ajaili ya kuwezesha uchumi wa familia na taifa.

“Njia za kisasa zina uhakika wa ufanisi kwa kuanzia asilimia 99 hadi asilimia 100 ikilinganishwa na njia za asili ingawa wataalamu wanaeleza kuwa kutokana na makosa ya binadamu na makosa yaliyo nje ya uwezo wa binadamu, ufanisi huo hupungua kidogo,” alisema.

Alisema kwa afya husaidia kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi, kuwapa nafasi ya kushiriki zaid katika shughuli za uchumi, kuwapa nafasi ya kujiendeleza na kuongeza ufanisi katika kufikia malengo ya jinsia na uwezeahaji kwa wanawake na wasichana.

Alisema  pia katika kuleta uwiano mziuri kati ya makundi ya jamii kati ya wazalishaji na wategemezi   kufikia malengo ya taifa uchumi.

Ofisa wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Kituo cha Mawasiliano ya Manedeleo Tanzania  (TCDC), Nazir Yusuph, alisema kwa mujibu wa Senza ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, kiwango cha elimu kati ya wanawake na wanaume wanaojua kusoma na kuandika, takwimu zinaonyesha wanaume ni asilimia 83 wakati wanawake ni asilimia 73.

Alisema pia takwimu za Kamisheni ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) zinaonyesha wanawake wa elimu ya juu ni asilimia 30 na katika kazi za umeneja na usimamizi wanawake ni asilimia 15 ikilinganishwa na wanaume, hivyo inaonyesha hakuna uwiano sahihi.

“Hii inaonyesha wanawake wengi wako katika sekta isiyo rasmi kwamba hawajaajiriwa kama wanaume wengi walivyoajiriwa hivyo wanajishughulisha katika shughuli za kujenga uchumi lakini ambazo hazihesabiwi na kuwafanya kubaki nyuma,” alisema.

Alisema  kwa sasa wanawake wanahitaji fursa katika elimu na kuwekeza katika shughuli za maendeleo hivyo inabidi kuwapo maelekezo ya kujikita katika uzazi wa mpango kwa sababu wasiofuatilia vizuri wanajikuta wakishindwa kushiriki kwa ukamilifu katika kujiendeleza na shughuli za maendeleo kwa kuwa hutumia muda mwingi kulea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles