Na ELIZABETH HOMBO-DAR ES SALAAM
BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA), limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika Oktoba na Novemba 2017, ambayo watahiniwa 287,713 sawa na asilimia 77.09 wamefaulu, huku waliopata daraja la nne na sifuri wakiwa ni asilimia 69.85.
Mwaka 2016, watahiniwa waliofaulu walikuwa 277,283 sawa na asilimia 70.07, takwimu zinazoonyesha kuwa ufaulu kwa 2017 umepanda kwa asilimia 7.
UDANGANYIFU
Akitangaza matokeo hayo jana Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde, alisema katika mitihani hiyo, udanganyifu umeongezeka ikilinganishwa na mwaka 2016.
Alisema kutokana na udanganyifu huo ambao ni pamoja na watahiniwa kuwa na mfanano wa majibu usio wa kawaida, mamluki kufanyiwa mitihani, huku wengine wakiandika matusi, watahiniwa 265 matokeo yao yamefutwa.
Dk. Msonde alisema kati ya watahiniwa hao, 136 ni wa kujitegemea na 129 ni wa shule.
Alisema mtahiniwa mmoja aliandika matusi katika karatasi yake ya majibu.
Mwaka 2016, watahiniwa ambao matokeo yao yalifutwa kwa sababu ya udanganyifu ni 87, kati yao wa kujitegemea wakiwa 25 na wa shule 55 na 10 wa mtihani wa maarifa (QT).
MAMLUKI KUWAFANYIA MITIHANI WATAHINIWA
Dk. Msonde alisema katika matukio ya udanganyifu yaliyojitokeza, ni pamoja na watahiniwa wa kujitegemea kukodi mamluki kwenda kuwafanyia mitihani wakati wenyewe wakiwa …………………………….
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA.