25.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

UBA Tanzania yasheherekea siku ya wanawake na wateja wake

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

Wafanyakazi wanawake wa Benki ya UBA Tanzania wamesherehekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa kuwaalika wateja wanawake kushiriki kifungua kinywa katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo, ikiwa ni kutambua mchango wa wanawake katika jamii.

Kaulimbiu ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake 2020 ni ‘Dunia sawa ni dunia iliyowezeshwa’. Kila mmoja kwa usawa.

Siku hii inayosherehekewa Machi 8 kila mwaka, inatoa fursa ya kutafakari maendeleo yaliyopatikana, kutoa wito wa mabadiliko na kusherehekea matendo ya ujasiri na uamuzi uliofanywa na wanawake wa kawaida ambao wametekeleza majukumu katika historia ya nchi zao na jamii.

Katika kuadhimisha siku hii maalumu ya wanawake Ijumaa ya Machi 6, UBA Tanzania ilitembelea wanawake wenye matatizo ya Fistula katika Hospitali ya CCBRT na kuchangia vifaa vya matibabu, pampas za wanawake watu wazima pisi 40.

Mbali na hivyo pia walitoa mafuta ya kujipaka 40, sabuni za kufulia pisi 40, dawa za meno pisi 40, miswaki pisi 40, sahani 100 na bakuli 50, vikombe vya chai pisi 100, kanga doti 100, vyandarua vya mbu pisi 100, dawa za mbu za kupuliza katoni 5, mabeseni 100, kandambili pisi 100 na taulo za kike pisi 40.

Wanawake wa UBA Tanzania walitekeleza jukumu lao muhimu kwa kuwawezesha pia wanawake wengine kupitia shughuli mbalimbali zilizofanywa na benki hiyo kusaidia wanawake na wanafunzi wa kike kwa kuwapatia taulo za kike, taulo za wajawazito na vifaa vingine.

Hata hivyo katika hafla iliyofanyika leo  jijini Dar es Salaam, Makao Makuu ya UBA Tanzania, Pugu Road jirani na Mfugale Flyover, timu ya viongozi wanawake wa benki hiyo  na wafanyakazi wengine wanawake walitoa elimu na kujadili masuala mbalimbali wanayopitia wanawake na mwisho walipata kifungua kinywa na wateja wote wanawake walioalikwa.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Ofisa Mkuu wa Uendeshaji wa benki hiyo, Flavia Kiyanga, aliwataka wanawake kujishughulisha katika shughuli za ujasiriamali na shughuli nyingine za biashara ili kujiwezesha na kujimarisha kiuchumi.

Naye Katibu wa Kampuni, Victoria Lupembe, aliwaeleza wanawake kuwa kwa sasa usawa wa kijinsia umefikia mahali pazuri katika kampuni nyingi, ikiwamo UBA Tanzania ambayo imeajiri idadi kubwa ya wanawake katika nafasi za utendaji na zisizo za utendaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles