24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

TWCC: Mwitikio wa wanawake kumiliki biashara umeongezeka

Derick Milton, Simiyu

CHAMA cha wanawake wafanyabiashara Tanzania (TWCC) kimesema kuwa kwa sasa kuna idadi kubwa ya wanawake kuanzisha biashara yao wenyewe kutokana na kupata fursa nyingi za mikopo, ujuzi, masoko na elimu kutoka serikalini pamoja na vyama vya kibiashara.

Chama hicho kimesema kuwa zamani wanawake walishiriki zaidi kwenye shughuli za kilimo, ambapo masuala ya biashara waliachiwa wanaume tu ambapo kwa sasa wanawake wengi wanamiliki biashara zao.

Hayo yamesemwa leo na Afisa wanachama kutoka chama hicho, Prosensia Mbunda wakati akiongea na Mtanzania Digital kwenye maonesho ya sikukuu ya wakulima kitaifa yanayofanyika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.

Mbunda amesema kuwa mpaka sasa chama hicho kimesajili wanachama wanawake ambao ni wafanyabishara 5000 nchi nzima, ambapo wote ni wanamiliki wenyewe biashara hizo.

“ Tunaona hata hapa kwenye maonesho ya Nanenane, wafanyabiashara wengi ni wanawake na wamejitokeza kwa wingi, hii inatufanya sisi kama chama kuendelea kufanya kazi ya utetezi na ushawishi kwa nguvu kubwa, na kuwasaidia wapate mikopo yenye riba nafuu,” amesema Mbunda.

Aliwataka wanawake wengi wajaslimali na wafanyabishara kujiunga na vyama vya kibiashara ikiwemo TWCC ili waweze kupata fursa za masoko, mikopo nafuu, ujuzi pamoja na elimu ya kuboresha kazi zao.

Kwa upande wake mmoja wa wajasliamali mwanachama wa chama hicho kutoka Mkoani Tabora Amina Madeleka, alisema changamoto kubwa ambao bado wanakabiliana nayo ni kutopatikana kwa vifungashio vyenye ubora unaotakiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles