24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Twanga kumpongeza Samatta leo

SamattaNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

BENDI ya muziki wa dansi, The African Satrs ‘Twanga Pepeta’, inatarajiwa kuangusha burudani katika shamrashamra maalumu za kumpongeza Mchezaji Bora wa Soka Afrika kwa wachezaji wa ndani, Mbwana Samatta zitakazofanyika leo kwenye Ukumbi wa Dar live, Mbagala Dar es Salaam.

Mbali na bendi hiyo, kutakuwa na burudani nyingine kutoka kwa waimbaji kama vile Khalid Chuma ‘Chokoraa’ aliyeimba wimbo maalumu wa kumpongeza mchezaji huyo, Msaga Sumu na Juma Nature.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mkurugenzi wa ukumbi huo, Juma Mbizo, alisema mgeni rasmi anatarajiwa
kuwa Mbunge wa Mbagala, Issa Ally akiambatana na viongozi mbalimbali wa jimbo hilo.

“Sherehe hizi zitakuwa ni za kumpongeza na kumuaga Samatta kuelekea safari yake ya kucheza soka barani Ulaya, hivyo kama wakazi wa Temeke ikiwa ni sehemu alipokulia tumeandaa burudani hii ili kushehereka naye kwa pamoja,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles