Gabo hana mpango na Wahindi

0
929

gabozagambaNA MWANDISHI WETU

MKALI wa filamu hapa nchini, Gabo Zigamba, amedai kwamba anaweza kusambaza kazi zake mwenyewe bila ya kuwategemea Wahindi.
Msanii huyo amedai kwamba filamu yake ya ‘Safari ya Gwalu’ alifanikiwa kuisambaza mwenyewe kupitia kampuni yake ya D Entertainment, hivyo hana ulazima wa kutegemea watu binafsi.

“Nilikuwa kama najaribu kuisambaza kazi hiyo mimi mwenyewe, nimegundua kwamba inawezekana kwa kuwa nimeweza kusambaza Tanzania mzima kupitia kampuni yang“u. Hivyo sioni sababu ya kuwategemea Wahindi
kuweza kusambaza kazi zangu, nimeuza kazi nyingi sana na bado watu wanaendelea kuzihitaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here