28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

TUCTA yavuta pumzi ajira za Serikali

Gratian-MukobaNa Veronica Romwald, Dar es Salaam

SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), limesema linaivutia pumzi hatua ya Serikali ya kusitisha kwa muda ajira mpya pamoja na kufuta vibali vya likizo bila malipo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Rais wa TUCTA, Gratian Mukoba, alisema wanasubiri hatua hiyo imalizike wapime ndipo watoe tamko lao rasmi.

“Tamko la Serikali limejieleza wazi kuwa wamefanya hivyo kwa nia ya kukabiliana na wimbi la watumishi hewa. Ukweli hata mimi nachukia kuona kuna watumishi hewa maana wanagharimu fedha nyingi na hivyo kufanya wafanyakazi kupata mishahara kiduchu, hususan walimu,” alisema.

Mukoba alisema kwa msingi huo ndiyo maana anaunga mkono hatua ya Serikali ya kuwakamata watumishi hewa inayoendelea kuchukuliwa hivi sasa kote nchini.

“Nakubaliana na kamata kamata ya watumishi hewa inayoendelea, naamini Serikali imefanya utafiti wa kutosha wa kukabiliana na hilo ili kuimaliza kabisa changamoto hiyo,” alisema.

Alisema TUCTA inatarajia kuwa baada ya Serikali kumaliza kuwaondoa watumishi hewa kwenye mfumo wa malipo, watapitia upya viwango vya mishahara na pengine kuiongeza.

“Hivyo ni mapema kuhoji kwamba kwanini hawaajiri… nisije nikatamka vitu ambavyo si sahihi, isiwe nikawalazimisha kuajiri wafanyakazi huku ikiwa haina fedha ya kutosha kulipa, maana watumishi hewa wamezimaliza.

“Kwahiyo tunasubiri wamalize mchakato wa kuwaondoa, watakapokamilisha hatua hiyo tutajipanga na tutatoa tamko letu rasmi,” alisema.

Akizungumza na MTANZANIA juzi, Katibu Mkuu Utumishi, Dk. Laurean Ndumbaro, alisema  Serikali imesitisha kwa muda utoaji wa ajira, ili kupitia upya muundo wa Serikali na taasisi zake.

Ndumbaro alisema Serikali imechukua hatua hiyo kama njia ya kukabiliana na wimbi la watumishi hewa nchini.

Alisema utekelezaji wa mkakati huo utakwenda sambamba na kusitisha kwa muda utoaji wa vibali vya ajira zote mbadala pamoja na uidhinishaji wa ajira hizo zilizopo Sekreterieti ya Ajira katika utumishi wa umma na kwenye mfumo wa taarifa za kiutumishi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles