23.5 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Jela maisha kwa kulawiti mtoto wake

REHEMA ABDALLAH (A3) NA HAMIDU ABDALLAH (DSJ), DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam, imemhukumu Msafiri Mchuno (28) kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wake mwenye umri wa miaka mitano (jina linahifadhiwa).

Mchuno ambaye ni dereva na mkazi wa Msimbazi, Dar es Salaam, anadaiwa kufanya unyama huo Februari 12, mwaka huu. Alimlawiti mtoto huyo na kumsababishia maumivu makali.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Juma Hassan, baada ya kukamilika kwa ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na upande wa mashtaka ambao ulikuwa na mashahidi watatu.

Awali Wakili wa Serikali, Grace Mwanga, aliitaka mahakama hiyo kutoa adhabu kali ili iwe onyo na fundisho kwa wote wenye tabia kama hiyo.

“Naomba mahakama impe adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hii kwani matendo haya yamekuwa mengi katika jamii, hususani huyu ni mtoto wake,” alisema Wakili Mwanga.

Awali akitoa utetezi wake mbele ya Hakimu Hassan, mshtakiwa huyo alishindwa kujitetea jambo ambalo lilisababisha mahakama kumwamuru kutumikia kifungo cha maisha jela.

Kwa mujibu wa ushaidi uliowasilishwa mahakamani hapo, Mchuno alimfuata mtoto huyo kwa bibi yake kwa ajili ya matembezi ya kawaida na alipomrudisha alibainika kufanyiwa ukatili huo na baba yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles