New York, Marekani
Maofisa nchini Marekani katika Jimbo la New York, wamesema wamelazimika kuchunguza madai kwamba Rais Donald Trump, amesaidia familia yake kukwepa kodi ya mamilioni ya Dola mwaka 1990.
Rais Trump, amemshutumiwa kwa kuhusika na mpango wa ubabaishaji pamoja na udanganyifu wa ulipaji kodi ili kuficha makadirio yanayomhusu yeye, ndugu na wazazi wake.
hata hivyo, Ikulu ya White House, imetupilia mbali madai hayo kuwa ni ya upotoshaji.
Msemaji wa White House Sara Sanders, ameongeza kusema malipo yote yalikuwa yakikaguliwa na kupitishwa na mamlaka za kodi kwa miaka mingi iliyopita.
Rais Trump, bado hajasema lolote kuhusu madai hayo lakini mwanasheria wake Charles Harder amekana vikali mteja wake kutenda kosa lolote.