28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Trey Songz amshangaza mama yake

Trey na mama yakeMSANII wa muziki wa RnB nchini Marekani, Trey Songz, amemshangaza mama yake kwa kumnunulia nyumba ikiwa ni zawadi kwa mchango wake kwenye muziki.

Msanii huyo amedai kwamba amepewa mchango mkubwa na mama yake katika kazi zake za muziki hadi kufika hapo alipo sasa, hivyo ameamua kumnunulia nyumba kama zawadi.

“Nimekuwa na jina kubwa kwenye muziki kutokana na mchango wa mama yangu, ninaamini bila yeye nisingekuwa hapa, hivyo nimeona bora nimnunulie nyumba kama zawadi yangu, najua nimemshtua sana kwa kuwa hakuamini,” aliandika Trey kwenye akaunti yake ya Twitter.

Hata hivyo, mama wa Trey alisema: “Najivunia mafanikio ya mwanangu, nashukuru kwa zawadi hii na kunikumbuka kama mzazi ambaye nimetoa mchango wa mafanikio,” alisema.

Mbali na Trey kumnunulia mama yake nyumba, pia Nasir Jones ‘Nas’ aliwahi kufanya hivyo baada ya kufanikiwa katika muziki huku akidai kwamba mama yake alikuwa na mchango mkubwa wa kumfikisha hapo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles