26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Rihanna alizwa na wimbo wake

RihannaaDUBLIN, IRELAND

MKALI wa muziki wa Pop, Rihanna, juzi alijikuta akidondosha chozi kwenye jukwaa wakati anaimba wimbo wake wa ‘Love the Way You Lie’.

Msanii huyo alikuwa kwenye ziara yake ya muziki nchini Ireland, katika shoo ambayo aliifanya juzi alijikuta akishindwa kumaliza kuimba wimbo wake na kuwaacha mashabiki wake wakiendelea kuimba.

Video ya msanii huyo wakati analia jukwaani ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii, hata hivyo mrembo huyo alipoulizwa nini kilikuwa kinamliza, alidai kwamba alikuwa na hisia kali kwa mashabiki wake.

Hata hivyo, kupitia akaunti yake ya Instagram, msanii huyo aliwaomba radhi mashabiki wake kutokana na hali hiyo.

“Siku zote muziki lazima uambatane na mashabiki, nawapenda sana na nashukuru kwa sapoti yenu katika maisha yangu ya kila siku, naomba radhi kwa mashabiki wa Ireland kwa kilichotokea,” aliandika Rihanna.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles