24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mke wa Rais Buhari amwita gavana mbwa kichaa

Aisha BuhariABUJA, NIGERIA

MKE wa Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari amemshambulia Gavana wa jimbo la Ekiti, Peter Ayodele Fayose kuwa yu mbwa kichaa baada ya kutuhumiwa ufisadi.

Gavana huyo wa upinzani alimtuhumu Aisha Buhari kuhusika na kashfa ya rushwa inayomhusu mwakilishi wa zamani wa Marekani, William J. Jefferson.

Mwaka 2009, Jefferson alitiwa hatiani kwa makosa 11 ya ufisadi na alipewa adhabu ya kifungo cha miaka 13 jela.

Mahakama nchini humo ilibaini kuwa alipokea rushwa ya dola 500,000 na akaunti yenye jina la Aisha Buhari nchini Nigeria ilitajwa wakati wa usomaji hukumu kama moja ya zile ambazo uhamishaji wa fedha kwenda kwa Jefferson ulifanyika.

Ofisi ya Rais ilipuuza tuhuma za Fayose huku msemaji wa rais, Garba Shehu akiziita kuwa za kitoto na ambazo zimelenga umaarufu katika vyombo vya habari.

Shehu alidai mke wa rais hahusiki na kesi ya Jefferson na alitoa changamoto kwa Fayose kutoa ushahidi.

Aliyekuwa Mkuu wa Tume ya Uchumi na Uhalifu wa Kifedha Nigeria (EFCC), Ibrahim Lamorde, aliliambia gazeti la Premium Times la hapa kuwa Aisha Buhari aliyetajwa katika kumbukumbu za mahakama ni mtu mwingine na si mke wa rais.

Akaunti binafsi ya Twitter ya Aisha Buhari katika kile kilichoonekana kujibu tuhuma za Fayose ilisomeka;“Imetosha Fayose. Mbwa kichaa ambaye hakufungwa mnyororo. Nimeshindwa kukaa kimya,” alisema.

Fayose ni mwanachama wa chama cha upinzani cha People’s Democratic Party (PDP), ambacho kilishindwa madarakani baada ya Buhari kumshinda aliyekuwa Rais Goodluck Jonathan katika uchaguzi wa Machi 2015.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles