22.5 C
Dar es Salaam
Saturday, June 22, 2024

Contact us: [email protected]

Wanaume waliobadilishana wake watibuana kenya

NAIROBI, KENYA

MAKUBALIANO yenye utata, ambayo wanaume wawili wa hapa walibadilishana wake zao baada ya mmoja kumfumania mwenzake akiwa na mkewe yametibuka.

Makubaliano yao yalitibuka hivi karibuni baada ya mwanaume aliyefumwa na mke wa mwenzake, Patrick Mangala (25) kutishia kutengua mkataba huo kwa sababu ya upweke unaomkabili sasa kutokana na kukimbiwa na mke huyo.

Mwendesha pikipiki huyo maarufu kama bodaboda wa mjini Kakamega, alimtishia maisha mume wa ‘mkewe’ kuwa angemtoa uhai iwapo hatamrudishia.

Lakini Ernest Anjeche (42), ambaye tayari anaishi na aliyekuwa mke wa mwenzie huyo, Susan amekataa kumrejesha baada ya kunogewa naye.

“Mimi na mwenzangu Mangala tulikubaliana kuwa kwa sababu alikuwa akitembea na mke wangu nikiwa kazini tukaona bora amchukue kabisa aishi naye.”

Hata hivyo, sifahamu tena kilichotokea kwa sababu yeye ndiye aliyerudi kwangu akimdai Susan eti mwenzake amemkimbia, alisema Anjeche.

Susan kwa upande wake amegoma kurudi kwa mumewe wa zamani akisema hakuwa mwaminifu na yu mdanganyifu mkubwa.

Anjeche, tayari ameripoti kisa hicho polisi akidai kutishiwa maisha na kuwa Mangala alikuwa ‘amekiuka mkataba.’’

“Lakini mke wangu mpya amekataa. Amesema hawezi toka hapa, atakaa tu hapa. Na mimi nikasema sawa, huyo mke aliyenitoroka akija na kutaka kukaa hapa anakaribishwa kwa sharti awe mke wa pili,” alisema Anjeche.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles