28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

TFF yasalimu amri kwa Yanga

Alfred-LucasNA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

SHIRIKISHO la soka Tanzania ‘TFF’, limesalimu amri kiaina kwa uongozi wa Yanga baada ya kubariki uchaguzi huo kuendelea kama ulivyopangwa na Kamati ya Uchaguzi ya Yanga ambapo utafanyika Juni 11 ukiwa chini ya uangalizi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF.

TFF ambao walipewa mamlaka ya kusimamia uchaguzi na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), ratiba yao ilielekeza uchaguzi huo ufanyike Juni 25 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Shirikisho hilo, Alfred Lucas, alisema kuwa uamuzi huo wa kubariki Yanga kuendelea na zoezi la uchaguzi ulifanyika kwa kuzingatia kanuni na sheria za TFF ili kufanikisha zoezi hilo.

“Rais Jamal Malinzi aliomba kukutana na Kamati ya Uchaguzi ya Yanga na ya TFF, lengo ni kumaliza tofauti zilizojitokeza baada ya kila kamati kutangaza kuwa na mamlaka ya kusimamia uchaguzi huo.

“Kinachotakiwa ni kufanikisha zoezi zima la uchaguzi na si kutunishiana misuli, ndio maana TFF kwa kutumia busara tumeona tubaki kama waangalizi katika uchaguzi huo,” alisema Lucas.

Lucas aliongeza kuwa TFF iliitaka Kamati ya Yanga iwashirikishe wagombea ambao awali waliondolewa  kugombea nafasi kwenye uchaguzi huo, baada ya kuchukua fomu kwenye Shirikisho hilo baada ya kutangaza taratibu.

“Majina yaliondolewa kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo kutokana na kuchukua fomu za kugombea TFF, tumekubaliana yarudishwe ili uchaguzi huo ufanyike kwa amani,” alisema Lucas.

Wagombea tisa ambao walichukua na kurejesha fomu TFF ni Aaron Nyanda na Titus Osoro waliokuwa wakiwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya mwaka 2010 inayotambulika serikalini hadi sasa.

Wengine ni Paschal Laizer, Edgar Chibula, Mohammed Mattaka, Mchafu Chakoma, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ Omari Said kutoka Zanzibar ambao wanawania nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji.

Aidha, Lucas alitangaza rasmi muda wa awali wa klabu kuanza kusajili kwa ajili ya msimu mpya wa ligi 2016/ 2017, ambapo itakuwa Juni 15 hadi Agosti 6 mwaka huu.

“Kwa mujibu wa kalenda hiyo timu ambazo hazishiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, zitaanza kutangaza wachezaji waliositishwa mkataba  Juni 15 hadi 30 mwaka huu huku timu zinazoshiriki ligi hiyo zitaanza kutangaza wachezaji waliowaacha.

“Klabu zitaanza kufanya pingamizi kati ya Agosti 7 hadi 14 kabla ya kuthibitisha usajili kwa hatua ya kwanza kati ya Agosti 15 na 19 na kusubiri hatua ya pili ya usajili itakayoanza Agosti 17 hadi Septemba 7 mwaka huu,” alisema Lucas.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles