23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mexime: Vincent ameacha pengo Mtibwa

mecky meximeNA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Mtibwa Sugar, Mecky Mexime, amesema kikosi chake kimepata pigo baada ya kuondoka beki wao, Henry Vincent ‘Dante’, ambaye juzi alisaini mkataba wa miaka miwili katika klabu ya Yanga.

Vincent ni mmoja wa mabeki wa kati waliofanya vizuri msimu huu ambaye alisajiliwa na klabu ya Mtibwa Sugar akitokea Ligi Daraja la Pili katika timu ya Lindi Kariakoo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mexime alisema Dante ameonekana kutokana na uwezo wake mzuri uwanjani, hivyo amewapisha wengine ambao atawatengeneza na kukuza vipaji vyao.

“Kuondoka kwa Dante kumetuachia pengo licha ya kwamba hiyo ni nafasi yake ya kuzidi kujitangaza lakini watapatikana wengine kama yeye ambao wataziba nafasi yake.”

Alisema kwa sasa hana haraka ya kukabidhi ripoti yake hadi pale timu nyingine zitakapokuwa zimemaliza utaratibu wao na yeye ndio ataanza mchakato huo.

“Mfano mzuri kwa Dante alivyoondoka inawezekana kwenye ripoti nilitoa mapendekezo yangu halafu timu nyingine inakuja kumchukuwa mchezaji hivyo nakuwa sijafanya kazi yoyote,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles