24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, July 7, 2024

Contact us: [email protected]

TARURA,TANROADS na Benki ya Dunia wakagua mradi wa ujenzi wa barabara

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff leo Julai 2,2024 ameshiriki katika ukaguzi wa mradi wa Ujenzi wa barabara ya Iringa – Kilolo akiambatana na TANROADS na ujumbe wa Benki ya Dunia.

Mradi huo ni sehemu ya Mradi wa uboreshaji wa barabara vijijini na ufunguaji wa fursa za kiuchumi na kijamii unaotekelezwa na TARURA na TANROADS.

Ujumbe huo wa Benki ya Dunia unatembelea Miradi ya RISE kuona kama utekelezaji wake unaendelea kulingana na Mpango wa utekelezaji uliokubalika na kuona changamoto katika utekelezaji kama zipo.

Mradi wa ujenzi wa barabara ya Iringa (Ipogolo)-Kilolo (33.61) ni wa kiwango cha lami unatekelezwa na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) na Mkandarasi China Henan Engineering Company.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles