23.8 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Kijaji: Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam ni mfano wa kuigwa

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji, amesema maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) ya mwaka huu ni ya mfano wa kuigwa kwa sababu yamekidhi viwango vya kimataifa.

Akizungumza leo Julai 2, 2024, mara baada ya kutembelea maonesho hayo, Dk. Ashatu alisema maonyesho hayo yamekuwa ya kimataifa kwa sababu waonyeshaji kutoka nje ya nchi wameongezeka tofauti na ilivyokuwa awali.

Amesema maonesho hayo yatatoa fursa mbalimbali kwa Watanzania kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara wa ndani na nje. Aliongeza kuwa nchi 26 zimeshiriki maonesho hayo na zitaonyesha bidhaa zao mbalimbali.

“Tayari tumewaahidi Watanzania kuwa nchi hii ni ya viwanda, hivyo kwenye maonesho haya kuna viwanda vingi vimeshiriki kwa lengo la kubadilishana uzoefu,” alisema Dk. Kijaji.

Dk. Kijaji alisema kesho wanatarajia kuudhuriwa na Marais wawili, ambao ni Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi, ambaye atafungua maonesho hayo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewakaribisha wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kuhudhuria kwa wingi ufunguzi wa maonesho ya 48 ya DITF.

Amesema katika ufunguzi huo kutakuwa na mabasi yaendayo kasi (UDART) ambayo yatafanya safari zake katika maeneo ya Mbande, Chamazi na maeneo mengine ya Mbagala kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa ya kufika kwenye maonesho hayo.

Chalamila alisema maonesho hayo yamebeba kauli mbiu mahususi ya kuwakaribisha wawekezaji kufika kwa wingi kuwekeza nchini, ambayo inasema “Tanzania ni eneo sahihi na salama kwa uwekezaji.”

Ameeleza kuwa suala la usafi katika kipindi hicho cha maonesho limepewa kipaumbele na wamejipanga kuhakikisha wilaya yote ya Temeke inakuwa safi huku wakizingatia mabadiliko ya tabia ya nchi.

“Tunahakikisha suala la ulinzi na usalama linaimarishwa zaidi, hivyo majambazi na wadokozi hawatakuwa na nafasi katika maonesho haya. Pia, kamera tulizofunga zitatusaidia kuwaona wahalifu wote,” alisema Chalamila.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles