31.2 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

TARI kuendelea na utafiti GMO

Asha Bani -Dar es Salaam

Serikali kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo nchini (TARI) imesema wataendelea na majaribio ya Teknolojia ya Uhandisi  Jeni (GMO) kwenye vituo vilivyotengwa maalum kwa utafiti huo.

Majaribio hayo ni pamoja na uhandisi Jeni  ya mahindi na mihogo yanayofanyika shamba la Makutopora mkoani Dodoma na kituo cha Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Kauli hiyo imetolewa leo Juni 28,  na Mratibu wa tafiti za bioteknolojia za kilimo nchini Dk. Fredy Tairo kutoka Taasisi ya utafiti ya TARI Mikocheni wakati akiwasilisha mada ya hali ya utafiti wa GMO nchini.

Dk.Tairo amesema kuwa watu na baadhi ya Vyombo vya habari walielewa vibaya kauli iliyotolewa na  serikali kwamba  ilitaka watafiti wafuate utaratibu uliopangwa kwa kupitia Idara ya Mazingira chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais.

Hata hivyo alisema GMO tayari imeruhusiwa katika nchi zaidi ya tano baada ya kujiridhisha na tafiti mbalimbali zilizofanywa, nchi hizo ni Afrika Kusini, Sudan,Burkina Faso, Ethiopia na Kenya ambao wapo katika hatua ya mwisho.

 Mratibu huyoCkatika mada yake ameeleza sababu na umuhimu wa serikali kufanya tafiti za GMO ili kukabiliana na Changamoto sugu zinazotokana na madiliko ya tabia nchi ikiwamo ukame, wadudu na magonjwa sugu ili kuongeza tija kwa wakulima.

Na kwa upande wa zao la Muhogo unaofanyika katika taasisi ya utafiti ya TARI Mikocheni hujibu Dar es salaam unalenga kuipa Kinga mihogo kupambana na magonjwa sugu ya Batobato kali na michirizi ya kahawai ambayo yanaathiri sana zao wakulima wa muhigo Afrika hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Naye mtafiti Emmanuel Sulle, ambaye ni Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu katika Chuo Kikuu cha Western Cape cha Afrika Kusini amesema kuna haja ya serikali kuongeza bajeti kwenye tafiti za kilimo nchini ili kuwezesha watafiti wetu kupatafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili wakulima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles