27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

TOL Gases yatoa gawio la bilioni 1/- kwa wanahisa

Mwandishi wetu-Dar es Salaam

Kampuni ya TOL Gases Limited, imetangaza kutoa gawio la Sh bilioni moja kwa wanahisa wake ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo kwa kipindi ha miaka 20 tangu walipoingia kwenye Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE).

Hayo yamesemwa leo Juni 28, na Mkurugenzi Mtendaji wa TOL Gases Limited,  Daniel Warungu wakati wa mkutano wa mwaka 2019 uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema kutokana na mageuzi makubwa ya kiutendaji  ambayo yamefanyika katika menejimenti hivi sasa wamekuwa wakijiendesha kwa faida na kwa mwaka wa fedha wa 2018 wamepata faida ambayo imewezesha kuanza kutoa gawio ikiwa ndio mara ya kwanza kufanya hivyo tangu mwaka 1998 walipoingia kwenye Soko la Hisa.

 “Kwa kweli hivi sasa tunajivunia kwani tunajiendesha kwa faida, na ndiyo maana leo tumekutana na wanahisa kutangaza kugawa gawio ambapo hisa moja ni Sh. 17.37, jumla ya gawio ambalo limetengwa kwa wanahisa ni Sh. bilioni moja.

“Tunawashukuru wanahisa wote, menejimenti na bodi ya wakurugenzi kwa namna ambavyo wameshirikiana kwa pamoja kuhakikisha kampuni yetu tunafanya vizuri kwenye kuuza bidhaa zetu katika soko,” amesema Warungu.

 Amesema katika kuhakikisha wanapata faida waliamua kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima na kuongeza uzalishaji wa bidhaa zenye ubora na matokeo yake leo wanajipongeza kwa mafanikio yanayokwenda sambamba na utoaji wa hisa kwa wanahisa wote.

Kuhusu mikakati yao amesema ni pamoja na kununua mitambo miwili na kuongeza magari kwa ajili ya kusafirisha bidhaa katika nchi za SADC pamoja na Afrika Mashariki na kufafanua katika uamuzi wa Serikali ya Awamu ya Tano kuhamasisha ujenzi wa viwanda umeisaidia kampuni yao kuongeza idadi ya wateja.

 “Tunalo soko la uhakika ndani ya nchi ya Tanzania, lakini pia tunafanya biashara zaidi ya kuuza bidhaa zetu kwenye nchi mbalimbali za Afrika. Hivyo katika kufurahia mafanikio yetu , tunakwenda pamoja na kuweka mikakati ya kujiimarisha zaidi,” amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni hiyo, Michael Shirima, amewahakikishia wanahisa wote kuwa wamejiridhisha na utendaji kazi wa menejimenti ya sasa ambayo inafanya kazi vizuri na wameanza kuona matumaini makubwa ya kufanya vizuri.

 “Tunawapongeza menejimenti yetu, huko nyuma kwa miaka mingi hatukuwa tunafanya vizuri na ndio maana hatujapata gawio lakini safari hii tunapata gawio, hata hivyo menejimenti tuliiuliza zaidi ya mara moja hili la gawio litakuwa kila mwaka au itakuaje, wametujibu kuanzia sasa itakuwa ni kila mwaka kwani wanakwenda vizuri,” amesema.

Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya TOL Gases Limited, Michael Shirima .
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles