Kiongozi mbio za Mwenge ataka Kiwanda cha Chai Mponde kifufuliwe

0
1435

Amina Omari, Lushoto

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa,  Mzee Mkongea Ally amewaagiza waliopewa dhamana ya kukifufua kiwanda Cha chai Cha Mponde kilichopo wilayani Lushoto mkoani Tanga kufanya hivyo haraka ili wananchi wapate soko la zao hilo.

Ameyasema hayo leo Juni 28,  wakati akikagua kiwanda hicho akiwa kwenye ziara ya mwenge ambao upo wilayani Bumbuli kukagua miradi ya maendeleo.

“Wananchi wanataka kuanza kuuza chai yao katika kiwanda hiki hivyo ucheleweshaji utawasababishia kuchelewa kupata maendeleo yao,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here