31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

TANZANITE YACHANGIA MIL 140/- KODI, TOZO

NA RAMADHANI HASSAN -DODOMA

KATIKA kipindi cha mwaka 2015 hadi 2017, Madini ya Tanzanite yamechangia kiasi cha Sh milioni 140.95 kutokana na kodi na tozo ya huduma inayotozwa kwa mujibu wa sheria ya ushuru wa halmashauri.

Aidha, katika kipindi hicho mgodi wa Tanzanite One, umefanikiwa kuchangia jumla ya Dola za Marekani 429,664 katika utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii kuzunguka mgodi huo.

Hayo yalielezwa jana bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati, Stanslaus Nyongo, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ester Mahawe, aliyetaka kujua kiasi gani cha fedha kimechangiwa na madini hayo katika mapato ya Mkoa wa Manyara.

Akijibu swali hilo, Nyongo, alitaja manufaa mengine yaliyopatikana kwa wilaya hiyo ni pamoja na fursa za ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kutokana na kuwepo kwa migodi katika eneo husika ambapo mgodi umetoa ajira kwa wafanyakazi 674 kati yao asilimia 93 ya walioajiriwa ni Watanzania na asilimia 7 iliyobaki ni wageni.

Aidha, alisema kati ya wafanyakazi hao walioajiriwa asilimia 21.81 wanatoka vijiji vinavyozunguka mgodi wa Naisinyai na Mererani.

Alisema ili kuhakikisha kuwa madini ya Tanzanite yananufaisha wananchi wa Simanjiro, Serikali imetoa tamko la kutaka shughuli zote zinazohusu madini hayo ikiwemo uendeshaji wa minada na ujenzi wa viwanda vya uchakataji wa madini hayo zifanyike katika eneo la Mirerani.

“Serikali imetenga eneo katika kijiji cha Naisinyai, Mererani ili kuwa maalumu la kiuchumi kwa ajili ya uanzishaji wa viwanda vya uchakataji ili kuvutia uwekezaji katika eneo hilo kwa kutoa vivutio mbalimbali kwa wawekezaji,” alisema.

Nyongo alisema Wizara hiyo itaendelea kuhamasisha wawekezaji wa viwanda vya kuchakata madini ya tanzanite kujenga viwanda katika eneo hilo.

Katika kutekeleza hilo kwa vitendo, Naibu Waziri huyo alisema Wizara imepata kiwanja katika eneo la EPZ ili kujenga kituo cha umahiri.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles