27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yashuka nafasi saba viwango FIFA

taifastarzNA ADAM MKWEPU, DA ES SALAAM

TANZANIA imeshuka nafasi 7 katika viwango vya soka vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho la soka Duniani ‘FIFA’ huku Argentina ikiendelea kuongoza.

Mei mwaka huu Tanzania ilipanda hadi nafasi ya 129 kabla ya kuporomoka hadi nafasi ya 136, huku  Kenya ikishuka nafasi 13 kutoka nafasi ya 102 hadi 129 wakati Uganda ikibaki nafasi ya 72 katika viwango hivyo.

Orodha hiyo iliyotolewa jana na FIFA, ilionesha kuwa Uganda inaongoza ukanda wa Afrika Mashariki na kati ikifuatiwa na Rwanda iliyopo nafasi ya 103, Ethiopia 125, Sudan Kaskazini 128, Kenya, Tanzania na Sudan Kusini 157.

Pia orodha hiyo ilionesha nchi ya Ivory Coast inaongoza Afrika kwa kuwa nafasi ya 36, ikifuatiwa na Ghana iliyokuwa nafasi ya 37 na Senegal iliyoko nafasi ya 41.

FIFA ilitaja Argentina kuwa kinara wa viwango vya soka duniani ikifuatiwa na Ubelgiji na Colombia huku nchi ya Tonga, Somalia na Eritrea zikiwa za mwisho kwenye orodha hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles