26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yafuzu Kombe la Dunia

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

TIMU ya soka ya Tanzania kwa watu wenye ulemavu, Tembo Warriors, imefanikiwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2022 zitazofanyika Uturuki baada ya leo Desemba Mosi, kuichapa Cameroon mabao 5-0 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mabao hayo yamefungwa na Alfan Kyanga aliyefunga mawili dakika 2,15, Ramadhan Chomole  dakika ya  18 na Frank Ngailo  dakika ya  36, 44.

Viongozi wa Wizara wakiongozwa na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa  na Katibu Mkuu wake Dk. Hassan Abbasi wakishangilia  ushindi wa timu ya Tembo Warrior baada ya kufuzu kuingia Kombe la Dunia  Oktoba 2022 nchini Uturuki.

Tembo Warriors imefuzu Kombe la Dunia baada ya kutinga nusu fainali ya michuano ya Afrika wa wenye ulemavu (CANAF 2021) inayoendelea jijini  ambapo imekuwa timu ya kwanza kufuzu kati ya  nne  zinazotakiwa kwa Afrika.

Mchezo huo umeshuhudiwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini, Innocent Bashungwa na Rais wa Mashindano hayo duniani  Mateus Wildack na viongozi wengine wa wizara hiyo.

Wachezaji wa Tembo Warriors wakishangilia baada  ya mechi kumalizika  

Akizungumza na waandishi wa habari  baada ya mechi hiyo, Bashungwa amewahakikishia  Watanzania kuwa Serikali itaendelea kuisaidia  timu  hiyo  katika maandalizi ya Kombe la Dunia ili iendelee  kufanya vizuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles