24.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wanahabari watakiwa kutoa elimu ya Uviko -19

Na Ashura Kazinja, Dar es Salaam

WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kuendelea kuielimisha jamii juu ya maswala ya Uviko-19 kwa kuandika habari sahihi  za kuaminika, zitakazo waondolea wananchi sintofahamu iliyopo.

Hayo yamebainishwa na Meneja Mradi wa shirika la ARTICLE 19, Moses Opiyo kwenye mafunzo ya siku moja yanayohusu namna ya kukabiliana na Uviko-19 iliyofanyika jijini Dare es salaam.

Semina hiyo iliandaliwa na Shirika la Article-19 kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyakazi wa vyombo vya habari Tanzania (JOWUTA), na Congress of Africa Journalist (CAJ) chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).

Opiyo amesema ni vyema waandishi wa habari wakawa wazalendo kwa kuandika habari sahihi zitakazowasaidia wananchi kuelewa habari muhimu kuhusu janga hilo na hivyo kusaidia kuweza kujilinda na kuepukana na madhara yatokanayo na ugonjwa huo.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa JOWUTA, Said Mmanga amewashauri waandishi wa habari kuendelea kuelimisha jamii juu ya janga hilo kwa kuandika taarifa ambazo bado hazijafahamika vyema kwa jamii ili iweze kuishi kwa usalama.

“Tuendelee kuelimisha jamii, kwani janga bado lipo, hivyo sisi kama nguzo ya nne wajibu wetu ni kuendelea kuelimisha jamii bila kuchoka” amesema Mmanga.

Kwa upande wake Katibu wa JOWUTA Suleiman Msuya amesema semina hiyo itawawezesha waandishi wa habari kuandika habari zenye uhakika kuhusu Uviko-19 na hivyo kuondoa utata juu ya chanjo, kutokana na upotoshaji uliopo.

“Sisi kama waandishi wa habari tuendelee kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kuchukua tahadhari kuhusiana na janga hili la Uviko-19, tuwaeleweshe wananchi kuwa corona bado ipo na kwamba wanatakiwa kuchukua tahadhari” amesema Msuya.

Hata hivyo Programu Ofisa wa ARTICLE 19, Sarah Wesonga amesema waandishi wa habari hawana budi kuandika habari sahihi kuhusiana na Uviko-19 ili kuweza kuondoa habari za upotoshaji na za uongo zinazoendelea katika mitandao ya kijamii.

“Zipo taarifa za uongo ambazo jamii yenyewe inazizusha tu, hususani katika nchi za Afrika, na sababu hizo nyingi zinafanana na nyingine za kupotosha ukweli uliopo, na hivyo kupelekea watu wengi kuathiriwa na janga hili la Uviko-19” amesisitiza Wesonga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles