27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yaanza vibaya Kombe la Netiboli Afrika

Na Mwandishi Wetu

TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Netiboli, Taifa Queens, imeanza vibaya michuano ya Kombe la Netiboli kwa nchi za Afrika baada ya kufungwa na Uganda ‘She Cranes’, magoli 77-29 katika mchezo wa ufunguzi, uliochezwa leo asubuhi Novemba 9, 2021 kwenye Uwanja wa Wanderers Sports Arena, Windhoek, nchini Namibia.

Katika mchezo huo, Taifa Queens imeanza robo ya kwanza kwa kufungwa magoli 20-7,robo ya pili 22-7, robo ya tatu 18-7 na robo ya nne 17-8.

Michuano hiyo inayoendelea nchini Namibia, inatarajia kufikia tamati Novemba 16,2021 ikishikisha jumla ya timu tisa ambazo ni mwenyeji Namibia, Botswana, Zambia, Zimbabwe, Tanzania, Kenya, Uganda, Malawi na Afrka Kusini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles