23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Mashabiki 30,000 waruhusiwa Stars vs DR Congo

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

SERIKALI kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, imewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu ya Taifa, itakapocheza na DR Congo baada ya kuruhusiwa kuingiza mashabiki 30,000 katika mchezo huo wa kufuzu kombe la Dunia 2022, utakaopigwa Alhamisi Novemba 11,2021 dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Novemba 9,2021, jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Hassan Abbas, amesema kuna wakati mashabiki wanakosa nafasi ya kuingia uwanjani kutokana na kuchezwa katika kipindi cha Covid 19, lakini kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), wamejenga hoja CAF NA FIFA na kuruhusiwa kuingiza idadi hiyo ya mashabiki.

“Tunahamasisha Watanzania, tujitokeze, sisi kama Serikali tunawahamasisha Watanzania tuje Mkapa tumeruhusiwa mashabiki 30,000 kwa uwezo wa uwanja wetu, tuwatie moyo vijana wetu na kila Mtanzania popote alipo apige dua na kuanzia sasa posti chochote kuitakia kheri timu,” amesema Dk. Abbas.

Aidha amesema kuelekea mchezo na Madagasca Novemba 14.2021, Serikali na Kamati ya Kuhamasisha Taifa Stars,watakodi ndege aina ya Airbus, itakayopeleka timu nchini Madagasca.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TFF, Willfred Kidao, ametaja viingilio vya mchezo huo kuwa ni sh 5000 VIP B na C, wakati mzunguko ni sh 3000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles