27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga yapeleka burudani Zanzibar

Na Mwandishi Wetu

KLABU ya Yanga imeamua kuwapelekea burudani ya soka mashabiki wake wa visiwani Zanzibar ambapo itacheza mechi mbili za kirafiki ikianza kucheza leo Novemba 9,2021 saa 2:15 usiku dhidi ya Mlandege FC kwenye Uwanja wa Amaan.

Wanajangwani hao wamewasili leo visiwani humo na mchezo wa pili watacheza dhidi ya KMKM, Ijumaa Novemba 12 kwenye Uwanja huo.

Yanga ambayo imeanza vizuri Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kushinda michezo yote mitano iliyocheza, inatumia muda huu wa mapumziko kujiimarisha kuelekea mechi zijazo za ligi hiyo.

Mchezo unaofuata wa Ligi Kuu, Wananchi hao watakuwa ugenini kuikabili Namungo FC kwenye Uwanja wa Ilulu, mjini Lindi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles