24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Samatta atoa kauli ya kibabe

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

NAHODHA wa timu ya Taifa, Taifa Stars Mbwana Samatta tayari amejiunga na kikosi hicho, huku akisema mchezo dhidi ya DR Congo utatoa taswira ya timu hiyo kuelekea kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2022 itakayofanyika nchini Qatar.

Taifa Stars itacheza na DR Congo, Alhamisi Novemba 11,2021 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, jijini Dar es Salaam ambapo mchezo wa kwanza uliopigwa Septemba,2021 nchini Congo, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Akizungumza baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam, Samatta amesema wanafahamu umuhimu wa michezo yote miwili, lakini mchezo wa Alhamisi ndiyo utatoa dira ya nafasi gani watakuwa katika kundi la michuano hiyo.

Amesema wachezaji wenzake walikuwa tayari kambini wakiendelea na maandalizi, anaamini timu imejiandaa vizuri na watapambana kuhakikisha wanapata matokeo wanayohitaji na kuwataka Watanzania kuendelea kuwaombea.

“Tunafahamu umuhimu wa michezo yote iliyobaki, ila mchezo wa Alhamisi tupo nyumbani na utatoa taswira ya kundi zima, naamini kile tulichokuwa tunakifanya tangu mwanzo wa mashindano na Watanzania walikuwa wanatuombea,” amesema Samatta.

Baada ya mchezo na DR Congo, Stars itasafiri kwenda kucheza na Madagasca, mechi itakayopigwa Novemba 14,2021 nchini Madagasca.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles