TAIPEI, TAIWAN
WANANCHI wa Taiwan wameamua ndoa iwe kati ya mwanamke na mwanamme nchini humo.
Hatua hiyo ni pigo kwa makundi ya watu wanaopigania haki za wapenzi wa jinsia moja, na waliobadilisha jinsia.
Kura hiyo ya maoni iliyofanyika juzi na kuandaliwa na makundi ya Kikristo, dini ambayo wafuasi wake ni asilimia tano ya idadi nzima ya watu nchini humo, inakwenda kinyume na uamuzi wa Mahakama ya Katiba wa Mei 2017.
Mahakama ilikuwa imewataka wabunge kuhalalisha ndoa ya watu wa jinsia moja katika kipindi cha miaka miwli ijayo.
Ingawa kura hiyo ya maoni inaangaliwa kama ushauri tu, lakini maoni hayo ya raia yanatarajiwa kuwashawishi wabunge watakapotakiwa kufanya uamuzi mwakani.
Wabunge wengi wanatarajia kuchaguliwa tena katika uchaguzi mwingine mwaka 2020.