23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

TACAIDS yahimiza wadau kuja na mawazo bunifu ya kutokomeza unyanyapaa

* Yakutana na wadau kuuhisha Mkakati wa Unyanyapaa na Ubaguzi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wadau wa masuala ya UKIMWI wametakiwa kuandaa mkakati wenye tija ili kuondoa unyanyapaa na ubaguzi kwa watu wanaoishi na VVU hatua itakayosaidia kufikia malengo ya kitaifa na kidunia ya kumaliza unyanyapaa na ubaguzi kwa WAVIU.

Washiriki wakifuatilia mada katika kikao kazi cha kupitia Mkakati wa Kupunguza Unyanyapaa na Ubaguzi katika Mwitikio wa UKIMWI nchini, kikao hicho kimefanyika jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Machi 17, 2022 katika kikao kazi cha kupitia mkakati wa kupunguza Unyanyapaa na Ubaguzi katika Mwitikio wa UKIMWI, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko amesema ubaguzi na unyanyapaa ni moja ya malengo ya kidunia ifikapo 2030 kusiwe unyanyapaa kwa mtu anayeishi na VVU. 

Amesema shughuli kubwa ya kikao hicho ilikuwa ni kuhuisha Mkakati wa Kitaifa wa Kupunguza Unyanyapaa na Ubaguzi kwa WAVIU ambao sasa umepitwa na wakati, na kwamba kutokana na mambo mapya yanayojitokeza, mkakati huo uliopo ni wa mwaka 2013-2017 hivyo wanahitaji kutengeneza mkakati mpya unaoendana na wakati wa sasa na yale mazuri yaendelezwe.

“Upatikanaji wa mkakati wenye kuleta matokeo sahihi utatokana na mawazo pamoja na  michango ya wadau watakaoshiriki katika kuandaa mkakati huu ambapo pia itasaidia wataalam elekezi kuja na mkakati wenye mawazo yenu.

“Huwezi kufanikisha jambo bila mkakati, hivyo mjione mnakazi kubwa ya kufanya ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mnaweka mawazo yenu vizuri kwenye mkakati huu ili kufikia malengo, mawazo yenu pia yatasaidia kuja na mkakati wenye mawazo yetu wenyewe ambao utakuwa rahisi kutekelezeka na kupata matokeo chanya,” amesema Dk. Maboko.

Washiriki wakifuatilia mada katika kikao kazi cha kupitia Mkakati wa Kupunguza Unyanyapaa na Ubaguzi katika Mwitikio wa UKIMWI nchini, kikao hicho kimefanyika jijini Dar es Salaam.

Ameongeza kuwa Tanzania kuna tafiti mbili zimefanyika ambapo utafiti wa kwanza ulifanyika mwaka 2013 uki9husisha mikoa mitano na utafiti wa pili umefanyika mwaka 2021 ukijumhisha mikoa 15 na Halmashauri 31 kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na UKIMWI (UNAIDS).

“Baadhi ya mambo yaliyotajwa katika utafiti huo ni pamoja na unyanyapaa wa mtu binafsi na unyanyapaa wa nje ambao jamii pamoja na familia wanamyanyapaa mtu anayeishi na VVU.

“Aidha katika utafiti wa mwaka 2021 hali ya unyanyapaa kwa mtu binafsi ulionekana kupungua kutoka asilimia 20.5(2013) hadi asilimia 6.2 (2021) unyanyapaa wa nje ulionekana kupungua kutoka asilimia 28 hadi asilimia 5.5(2021).

“Hivyo, kwa kutumia yale yaliyokwenye mkakati wa kwanza wa ubaguzi na unyanyapaa wa mwaka 2021 pamoja na uzoefu na mambo mbalimbali tuyaweke pamoja ili tupate mkakati wa pili wa kupunguza unyanyapaa na ubaguzi utaoleta mafanikio katika mapambano haya,” amesema Dk. Maboko.

Washiriki wakifuatilia mada katika kikao kazi cha kupitia Mkakati wa Kupunguza Unyanyapaa na Ubaguzi katika Mwitikio wa UKIMWI nchini, kikao hicho kimefanyika jijini Dar es Salaam.

Ameongeza kuwa takwimu za mwaka 2021 kwenye ubaguzi wanje inaonekena mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa asilimia 19.5, kwa ubaguzi na unyanyapaa, ukifuatiwa na Tanga asilimia 10.5.

“Upatikanaji wa mkakati huu utasaidia kutuongoza ni mikoa gani tuanze nayo utekelezaji, ubaguzi wa ndani ambao ni asilimia 6.4 ambapo mkoa wa Geita ni asilimia 27, Mtwara asilimia 26.6 na Tanga asilimia 17, kwa kutumia takwimu hizi zitatusaidia kuona wapi tuanzie katika utekelezaji wa mkakati huu baada ya kukamilika,” amesema Dk. Maboko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles