24.3 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Sumatra kutoa utaratibu mpya

sumatraNa LEONARD MANG’OHA -DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra),imepanga kuanzisha utaratibu utakaowawezesha abiria wanaotumia mabasi ya mwendokasi kutoka Mbezi, kutumia tiketi moja hadi Hospitali ya Taifa Muhimbili kupunguza gharama wanazotozwa abiria wanaotumia usafiri huo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mkurugenzi wa Sumatra, alisema mpango huo ambao bado uko kwenye mchakato utamwezesha abiria kutumia nauli ya Sh 800 anayolipa kituo cha Kimara, kutumika hadi Muhimbili bila kulipa nauli nyingine.

“Kuna ‘proposal’ tunaiandaa kuwezesha abiria wanaotumia mabasi haya wakishuka kwenye kituo cha Gerezani wachukuliwe na mabasi yatakayoanzisha safari ya kwenda Muhimbili ili yawafikishe huko,” alisema Kahatano.

Alisema amefuatilia na kugundua mabasi hayo yamekuwa yakitoa huduma kwa kiwango cha kuridhisha katika kituo cha Mbezi Mwisho na kila baada ya dakika tano hadi 10, basi moja limekuwa likiwasili kituoni hapo.

Kuhusu upungufu wa daladala za kwenda Muhimbili, Kahatano alisema hakuna upungufu kwa sababu mzunguko uko kama kawaida.

Meneja Mawasiliano wa Sumatra, David Mziray, alisema mabasi yanayotakiwa kutoa huduma ya usafiri katika barabara ya Morogoro ni yale yaendayo kasi, baada ya Serikali kuanzisha mpango wa kupunguza msongamano wa magari katika barabara hiyo.

Alisema pamoja na kusimamishwa daladala binafsi kutoa huduma, mamlaka hiyo imeamua kuongeza muda kwa daladala zinazokwenda Muhimbili kuendelea kutoa huduma kutokana na barabara hiyo kutotumiwa na mradi wa barabara za mabasi yaendayo kasi.

Licha ya mamlaka hiyo kudai hakuna upungufu wa daladala za zinazokwenda Muhimbili,MTANZANIA lilishuhudia baadhi ya wananchi wakisota kituoni hapo kwa zaidi ya saa moja wakisubiri daladala, huku wengi wao wakieleza kushindwa kumudu gharama za kupanda mabasi ya mwendo kasi.

“Ili ufike Muhimbili unatakiwa upande basi hapa hadi Kimara kwa Sh 400, hapo tena upande basi jingine hadi Fire kwa Sh 650, ukishuka upande gari la Muhimbili hadi unafika umetumia Sh 1,450.

“Hivi kwa kipato gani hasa tulichonacho ua ndiyo wanataka turudi vijijini,” alihoji mmoja wa abiria aliyekuwa kituoni hapo. Meneja Uhusiano wa Umma, Wakala wa Mabasi yaendayo kasi, William Gatambi aliliambia MTANZANIA kuwa nauli inayopaswa kulipwa ni Sh 400 kwa mtu mmoja anayetoka Mbezi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles