30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

ACT WAZALENDO YAMSHANGAA RC KAGERA

meja-jenerali-mstaafu-salum-kijuuPATRICIA KIMELEMETA NA CHRISTINA GAULUHANGA

SIKU mojaa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu kuwaamibia wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi la hivi karibuni mkoani humo, wajitegemee  na kwamba misaada yote iliyotolewa ni ya Serikali na taasisi zake tu, kauli hiyo imewashangaza viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Taarifa iliyotolewa  Dar es Salaam jana na  Katibu wa Taifa wa chama hicho, Kamati ya Maendeleo ya Jamii, Janeth Rithe ilisema kauli hiyo haikubaliki kwa sababu  inadhalilisha waathirika na taasisi zote zilizojitokeza   kuwasaidia waathirika hao.

Alisema chama hicho kimeshtushwa na kauli hiyo na kuichukulia kama ni tangazo halali la wizi wa uaminifu wa mali za wananchi zilizotolewa na taasisi mbalimbali   kuwasaidia waathirika wa tetemeko hilo.

“Kauli iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali mstaafu, Salum Kijuu, hatuwezi kuiunga mkono kwa sababu inadhalilisha waathirika wa tetemeko la ardhi.

“Ikumbukwe  tangu tetemeko hilo litokee, taasisi na wananchi mbalimbali walijitokeza kuwasaidia waathirika hao, kwa nini sasa  wanashindwa kupewa mali zao na badala yake zinatoka kauli kama hizo? Hatuwezi kuunga mkono,”alisema Janeth.

Alisema  ni busara ya kawaida kuwa hatua ya kwanza katika kushughulikia maafa ni kurudisha hali ya maisha ya watu katika hali ya kawaida sambamba na ukarabati wa miundombinu.

Alisema suala la ujenzi wa miundombinu ya taasisi za umma, ni jukumu la msingi la Serikali ambalo haiwezi kulikwepa.

Alisema    chama hicho kimeitaka Serikali kuu kujitenga na kufuta kauli ya mkuu wa mkoa wa Kagera kwa sababu inaweza kusababisha migongano baina ya wananchi na serikali yao.

Serikali inapaswa kuelekeza misaada iliyotolewa ikiwamo michango kwa waathirika wa tetemeko hilo kama ilivyokusudiwa, alisema.

Rithe alisema  chama hicho kimetoa wito kwa taasisi za  raia   nchini kuchukua nafasi yake katika kuendelea kuikumbusha serikali wajibu wake wa msingi wa kuboresha maisha ya watu.

Alisema Watanzania wanakumbuka  Septemba 10, 2016 lilitokea tetemeko la ardhi   Kanda ya Ziwa na hususan Mkoa wa Kagera, ambalo lilisababisha baadhi baadhi ya wananchi kufariki na wengine kulazwa, huku nyumba na mali zao zikiharibika vibaya.

“Tetemeko hilo lilisababisha athari mbalimbali vikiwamo vifo, majeruhi, uharibifu wa makazi na miundombinu ya umma na watu binafsi, takwimu zilizotolewa na  mkuu wa mkoa huo, zilionyesha watu 117,721 waaliathirika kwa kupoteza makazi yao,”alisema.

Alisema nyumba 2,072 za makazi zilianguka na 14,595 zilibomoka, baadhi zilipata nyufa hivyo kuzifanya kuwa hatarishi kwa makazi ya binadamu.

Kutokana na hali hiyo, taasisi mbalimbali,  nchi marafiki, waliitikia wito wa kuwasaidia waathirika wa maafa na kukarabati miundo mbinu iliyoharibika, alisema.

“ Hadi kufikia  Oktoba, mwaka huu, f edha, vyakula na vifaa mbalimbali vya ujenzi vilikuwa  vimepatikana kwa njia ya michango mbalimbali,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles